← JamboSender

Sera ya Faragha / Privacy Policy

Ilisasishwa / Last updated: 2026-09-11

Kiswahili

JamboSender ni huduma ya Jambofix inayowezesha taasisi kutuma ujumbe wa SMS kwa wanachama, wazazi au wateja wao. Orodha za majina na namba za simu zinazopakiwa na taasisi zinabaki mali ya taasisi hiyo. Zinaonekana kwa watumiaji wa taasisi hiyo tu na kwa wasimamizi wa mfumo kwa madhumuni ya msaada wa kiufundi.

Hatuuzi, hatukodishi wala kushirikisha namba za simu na mtu yeyote. Namba hutumika tu kuwasilisha ujumbe ulioombwa na taasisi kupitia mtandao wa huduma za SMS. Taarifa za akaunti (jina, barua pepe, simu) hutumika kuendesha huduma na kuwasiliana nawe kuhusu akaunti yako.

Taasisi inaweza kufuta orodha zake wakati wowote kupitia mfumo, na inaweza kuomba kufungwa kwa akaunti na kufutwa kwa taarifa zake kwa kuwasiliana nasi.

English

JamboSender is a Jambofix service that lets organisations send SMS messages to their members, parents or customers. Contact lists uploaded by an organisation remain that organisation's property. They are visible only to that organisation's users, and to platform administrators for technical support.

We do not sell, rent or share phone numbers with anyone. Numbers are used solely to deliver the messages the organisation requests through our SMS gateway. Account details (name, email, phone) are used to run the service and to contact you about your account.

An organisation can delete its lists at any time in the portal, and can request account closure and deletion of its data by contacting us.